T.I COULD FACE LONG YEAR JAIL SENTENCE FOR DRUG CHARGES…!!!

T.I.’s arrest for drug possession on Wednesday could get the hip-hop icon back in jail, says Steven Knowles, a lawyer not representing the “Got Your Back” rapper

T.I. and his wife, Tameka Cottle, were arrested in West Hollywood, the Los Angeles County Sheriff’s Department told the Associated Press. Deputies pulled their car over after smelling marijuana and arrested them on suspicion of possessing meth amphetamines.

The trouble comes at a pivotal moment in T.I.’s career and personal life. His film Takers, which he acted in as well as co-executive produced, opened in theaters at No. 1 last weekend. His album, ironically called King Uncaged, is scheduled for a September 28 release. He just married Cottle in July, and was released from a halfway house in March.

This could put his life on hold.

Lawyer Steven Knowles suspects that, if convicted, T.I. could face a multiple-year jail sentence. “This is big-time,” Knowles told Yahoo! Music. “I really don’t envy his defense lawyer.”

Prior to serving three months in the halfway house, T.I. spent seven months in a federal prison in Arkansas for illegal firearms possession and possessing a gun as a convicted felon.

According to the Associated Press, as a condition of his three-year-parole, he was forbidden from committing another federal, state or local crime, or illegally possessing a controlled substance. Drug tests and participation in a drug and alcohol treatment program were also required.

The new allegations will not be taken lightly, said Knowles, a family attorney who has represented Britney Spears and Nicole Kidman, among others. “[T.I.'s] celebrity is not likely going to get him off of this,” he said. “This is now a repeated offense. That’s when even the celebrity get-out-of-jail card is not going to work.”

Knowles believes T.I.’s celebrity will probably ensure a more stringent ruling. “In fact, for them to take it light on him now would look like over-favoritism because he’s a celebrity, and I think, if anything, his celebrity may actually backfire.”

Knowles believes that Cottle, co-star of BET’s Tiny & Toya and a member of the ‘90s R&B group Xscape, could avoid jail time because of their children. “That is a big factor when it comes to sentencing,” he said. “I can tell you from my experience as a family lawyer that celebrity or not, courts loathe to jail moms, particularly if there’s not going to be a dad at home to care for the kids as well. This would mean kids would have no parents.”

One important factor in determining a potential sentence will be the quantity of drugs in possession. “If [the] quantity is large enough to be selling or even sharing with third parties, that could make a big difference,” Knowles said.

Filed under: Uncategorized | No Comments

WAZIRI MKUU KATIKA MKUTANO WA MAPINDUZI YA KILIMO NCHINI GHANA..!!!

Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akifurahia jambo na Rais wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuendeleza Kilimo (IFAD) Bw. Kanayo Nwanze (kushoto), kabla ya ufunguzi wa Mkutanowenye lengo la kuleta Mapinduzi ya Kilimo Barani Afrika (African Green Revolution Forum – AGRF) jijini Accra, Ghana leo asubuhi Septemba 2, 2010.

Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akimsikiliza Makamu wa Rais wa Ghana, Mhe. John Dramani Mahama wakati wa mjadala uliohusu Njia za Kufanukisha Mapinduzi ya Kilimo kwenyeMkutano wenye lengo la kuleta Mapinduzi ya Kilimo Barani Afrika jijini Accra, Ghana leo asubuhi Septemba 2, 2010. Kushoto ni Bw. Kofi Annan ambaye ni Mwenyekiti wa Alliance for a Green Revolution in Africa.

Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na Mwenyekiti wa Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), Bw. Kofi Annan (kushoto) wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Ghana, Mhe. John Dramani Mahama wakati akitoa hotuba ya ukaribisho kwenye Mkutano wenye lengo la kuleta Mapinduzi ya Kilimo Barani Afrika jijini Accra, Ghana leo asubuhi.

Rais wa zamani wa Nigeria, Mhe. Olesegun Obasanjo (kulia) akijibu swali wakati wa mjadala maalum kwenye Mkutano wenye lengo la kuleta Mapinduzi ya Kilimo Barani Afrikauliofunguliwa leo asubuhi (Septemba 2, 2010) jijini Accra, Ghana. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Ghana, Mhe. John Dramani Mahama na kulia ni Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda wakimsikiliza.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Filed under: Uncategorized | No Comments

PALE UNAPO KUTANA NA USIOYATARAJIA…..!!!!

Kijana mmoja aliyekuwa anasomea maswala ya ndege wa rukao angani alikuwa anajitayarisha usiku kucha kwa ajili ya mtihani siku inayofuatia.


Siku iliyofuata alikaa mbele kabisa katika chumba cha mtihani mbele yake kulikuwa na ndege sita waliokuwa wamefunikwa na kuachwa sehemu ya miguu tu.


Mwalimu akawambia wanafunzi kwa kuangalia miguu ya hawa ndege tambua kila mmoja ni ndege wa aina gani?


Yule mwanafunzi akamshangaa mwalimu na kujiuliza kukesha kote kule huu ndio mtihani wenyewe nitawezaje kuwatambua ndege kwa kuangalia miguu na wakati yote inafanana alijiuliza kwa mshangao mkubwa.


Huku akiwa mwenye hasira akamfuta mwalimu na kuumuliza Huu ndio mtihani gani?? huku akionyesha kuchanganyikiwa, sasa mtihani sifanyi utafanya mwenyewe huku ni kutaniana bwana aliongeza alafu akaondoka zake.


Lakini kabla hajafika mlangoni mwalimu akamsimamisha na kumuuliza Kijana subiri kwanza jina lako waitwa nani??, Yule kijana kwa hasira akamfuata na kupandisha suruali juu na kumwambia angalia miguu yangu utajua naitwa nani alafu akaondoka zake, darsa zima likagubikwa na kicheko!!

Filed under: Uncategorized | No Comments

MAO RWANGISA NA SOFIA NKURLU WAMEREMETA NEW YORK CITY…!!!

Bi Harusi Sophia Nkurlu akisindikizwa na Mpambe wake Sonia kuingia kwenye gari kuelekea kanisani.

Bi Harusi Sophia Nkurlu akishuka kwa limo pamoja na Mpambe wake Sonia.

Bi harusi akipelekwa kukabidhiwa  rasmi na kaka yake mkubwa Ephraim Nkurlu kwa Bw harusi Mao Rwangisa.

Wapambe nao walipendezaaaaaaa

Mao Rwangisa akikabidhiwa rasmi mtoto na mchungaji.

Mzee anasepa nao huyoooooooooo mpaka Bukoba.

****************

Blog Team: MO BLOG inawatakia Bwana na Bibi Harusi kila kheri katika maisha yao ya ndoa na wazae matunda mema pia inakukaribisha wewe mdau kukutumia picha zako za sherehe mbalimbali tuma picha zako na maelezo kamili kwenda mohammedewji@gmail.com

Filed under: Uncategorized | No Comments

HII LAZIMA ITAKUWA HUJUMA…!!!

Walianza kwa kusema kuwa hatutaweza ya kwamba ni ngumu kwa sisi kuandaa shindano kubwa kama hilo baada ya kuona tumeweza wakaja na kasoro nyingine ambazo mpaka shindano linamalizika wenyewe walibaki midomo wazi hawana cha kusema sana sana waliposhudia  fataki zikirindimba siku ya ufungaji wa mashindano hayo pale Soccer City. Nadhani wote mmejua nazungumzia mashindano gani? ni kombe la dunia 2010 lililofanyika Afrika ya Kusini.

Lakini katika kombe hilo kitu kilicholifanya likaonekana nila pekee ni jinsi ya ushangaliaji uliokuwa ukipendezeshwa na mavuvuzela mpaka kufikiwa kifaa hicho kupewa tuzo ya utambulisho pekee wa mashindano hayo.Hakika  katika kudhihirisha upenzi wa kifaa hicho mpaka mashabiki toka nchi mbalimbali walitokea kuvutiwa na vuvuzela wadogo kwa wakubwa hadi ngazi ya viongozi wa nchi.

Tumeamua kusema hujumaa ni baada ya baadhi ya vyama mbalimbali kutoka nchini ulaya kupiga marufuku ushangiliaji kwa kutumia mavuvuzela wakidai eti niusumbufu kwa wachezaji !!. Lakini shirikisho la mpira wa miguu barani ulaya UEFA wao ndio wameamua kuweka wazi kwamba hawataki vuvuzela kuhofia kuharibu utamaduni wao. Hili linaonyesha wazi kwamba vuvuzela ingeruhusiwa katika viwanjan vya ulaya basi utamaduni wa mwafrika ungeshika kasi kwa sasababu chanzo cha kifaa hicho ni huku Afrika. Hii ikionyesha wazi yakuwa utamaduni wa mwafrika au mtu utaendelea kukanyagwa na watu wa ulaya.

Filed under: Uncategorized | No Comments

KIAMA CHA WACHAKACHUAJI MAFUTA CHA TIMIA…!!!

Magari mengi yamekuwa yakiharibika na hata kufa baada ya mda mfupi kutokana na kuwekewa mafuta yalio chakachuliwa (Kuchanganywa na mafuta ya taa) na hali imekuwa ikiwagharimu sana wamiliki wamagari hapa nchini. Na kwa upande wa serikali imejikuta ikipoteza mapato mengi yanayofikia mpaka bilioni 100 hadi 200 hiyo ni hadi mwezi wa sita mwaka huu kutokana na kamchezo hako ambapo lengo lake kubwa ni kuwaingizia faida wafanyabiashara wa bidhaa hiyo.

Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA) sasa wamekuja na dawa maalumu itakayo kuwa ikitumika kukagua visima vya mafuta kama mafuta hayo yamechakachuliwa au la. Dawa hiyo yenye asili ya kimiminika ilianza kutumiwa katika kampuni ya Oryx iliyoko Dar es Salaam. Mkurugenzi wa mamlaka hiyo alisema kuwa hatua hiyo so ya mda maalumu bali ni endelevu ampapo visima vyote vya mafuta nchini vitakuwa vikikaguliwa kabla bidhaa hiyo haija ingia sokoni.

Blog team: Kweli kufa kufaana, wakati wamiliki wa magari wanaingia hasara ya magari yao kufa kutokana na mafuta mabovu upande wapili wa shilingi wauzaji ndio wanapata faida!!. Kisheria huu ni ukiukwaji wa msharti ya uuzaji wa bidhaa ambapo ni jukumu la muuzaji kujali maslahi ya mteja anaeenda kutumia bidhaa au huduma yake.

Filed under: Uncategorized | No Comments

THE TOP TEN OF EVERYTHING….!!!

To be Continue….!!!

Filed under: Uncategorized | No Comments

WASWAHILI HUSEMA ULIMI HAUNA MFUPA…..!!!

Msemo huo husemwa sana pale mtu anapokuwa amekosea kutamka neno au kutamka neno ambalo hakulimaanisha kwa wakati ule.

Msemo huu umemkuta mbunge wa Handeni Tanga Dk.Abdallah Kigoda baada ya bila kujifahamu alijikuta akimnadi aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Bw. Benjamin William Mkapa kwa kusema (Mkapa Oyeeee….!!!) badala ya mgombea urais wa sasa kupitia chama tawala CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Dk.Kigoda alikutwa na mahasibu hayo wakati wa ufunguzi wa kampeni za mgombea ubunge kupitia chama hicho jimbo la Kilindi Bi. Beatrice Shelukindo zilizofanyika katika kijiji cha Kwediboma.

Blog Team: Sisi hatuna cha kucomment, kama wewe mpenzi wa MO BLOG Unacho tuambie unapata picha gani?

Filed under: Uncategorized | No Comments

SISI KAMA WAMILIKI WA MAGARI TUNAJIFUNZA NINI?

Ni hivi karibuni tu jeshi la polisi nchini kwa kushirikiana na makao makuu ya shirikisho la Kimataifa la polisi (Interpol) limekamata magari 51 yaliyoibiwa kutoka nje ya Tanzania na baadaye kuingizwa nchini katika operesheni maalum iliyofanyika kati ya August 27-28 mwaka huu kwa ajili ya kuwasaka, kuwatambua na kuwakamata  wahalifu mbalimbali nchini.

Taarifa ya polisi ilisema magari 22 miongoni mwa hayo yaliibiwa Japan, 12 Afrika ya kusini na 3 yaliibiwa nchini Uingereza na gari  1 nchini Kenya, Malaysia 8, Slovania 1 , Ujerumani 1, Msumbiji 1, na moja Tanzania. Ambapo magari 10 yalionekana na kasoro kadhaa ikiwamo nyaraka na chesisi tofauti.

Blog Team: Tunapenda kutoa pongezi zetu za dhati kwa jeshi la polisi nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya. Lakini ingekuwa ni vizuri kama ingetolewa elimu kwa wadau wanaomiliki vyombo hivi vya usafiri ni kwa jinsi gani wataweza kuepukana na janga hili la kuziwa magari ya uwizi.

Filed under: Uncategorized | No Comments

AY; NAZIDI KUVUKA BODA WATANZANIA NAOMBA KURA ZENU…!!!

Kwa mwaka huu AY alianza kunyakua tuzo ya Chaguo la Teneez ya Kenya,Kili Awards ya Tanzania na Museke Awards ya Ghana.Mwaka huu ni moto chini sidhani kama kuna artists wa bongo aliyekuwa nominee kwa awards za nchi tofauti na kushinda Tuzo..

Sasa amechaguliwa katika final za Tuzo za Ufaransa za RADIO FRANCE INTERNATIONALE DISCOVERIES AWARD 2010 {Rfi Prix Découvertes 2010} zitazofanyika September,ndani ya Paris.AY anawaomba watanzania wote kumpigia kura za kutosha aweze/tuweze kushinda tuzo hizo.Unaweza kuvote kupitia www.rfimusique.com

Filed under: Uncategorized | No Comments

KAMBI YA VODACOM MISS TANZANIA YAPATA MAFUNZO KUTOKA KWA VIONGOZI WA WIZARA YA HABARI,MICHEZO NA UTAMADUNI…!!

Mkurugenzi wa Kamati ya mashindano ya  Vodacom Miss Tanzania Hashimu Lundega (kushoto) akiwatambulisha Viongozi wa Wizara ya Habari michezo na Utamaduni wakati walipotembelea kambi ya miss Tanzania iliyopo katika Hoteli ya Giraffe wapili kutoka kushoto Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Tanzania Hermas MwasoKo, Mkurugenzi msaidizi anayesaidia Sanaa wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo ANNA NGOI.Afisa Utamaduni Mkuu wa Wizara hiyo Chiku Shomari.Viongozi hao walitembelea kambi hiyo ili kuwapa ushauri mablimbali ikiwemo na kuwahamasisha kujiamini katika shindano la miss Tanzania litakalofanyika Septemba 11 mwaka huu.

Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo nchini Hermas MwasoKo  akiwapa hamasa warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania katika Hoteli ya Giraffe ambapo viongozi wa Wizara hiyo walitembelea kambi ya Miss Tanzania kwa nia ya kujionea na kutoa ushauri kwa warembo hao.(kulia) Mkurugenzi Msaidizi anayesaidia Sanaa katika Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Anna Ngoi,(kushoto) Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashimu Lundenga.

Afisa Utamaduni Mkuu wa Wizara ya Habari na Utamaduni Chiku Shomari akisisitiza jambo kwa Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010.ambapo aliwataka warembo hao kujiona kuwa wao ni kioo cha jamii hivyo wajiheshimu na kujitunza ili wawe mfano kwa wengine,(Kulia) Miss Tanzania 2009 Miriamu Gelard kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anaye saidia Sanaa Anna Ngoi.

Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi  wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari utamaduni na Michezo Hermas Mwasoko. wakati alipowatembelea kambini kwao katika Hoteli ya Giraffe Dar es Salaam

Mkurugenzi Msaidizi anaye saidia Sanaa Anna Ngoi (kulia) akisalimiana na baadhi ya Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania Septemba 11 mwaka huu, baada ya kumalizika kwa kuwapa ushauri katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Giraffe.

Filed under: Uncategorized | No Comments

MCHEZO WA TENNIS WAFIKIA ROBO FAINALI – GYMKHANA..!!!

Wacheza Tennis wakiendelea na mchezo huo katika Viwanja vya Gymkhana walipokuwatwa na mpiga picha wetu.

Baadhi ya wacheza Tennis wakiwa wamekaa Bench wakifuatilia mchezo ambao uliokuwa ukiendelea hapo uwanjani.

**********************

Mchezo wa tennis wa Ligi ya Simba Cement umefikia hatua ya robo fainali ambapo wanaume wamebaki 32 huku kwa upande wa wanawake wakibaki 14 na Vetenari wakiwa 16,pia  mashindano haya yamejumuisha nchi mbalimbali ambapo fainali za mchezo huo zinatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi tarehe 4/9/2010 ambapo mshindi ataondoka na kitita cha US $1000 kitakachotolewa na kampuni ya Simba Cement hayo yamesemwa leo na Kocha ambaye pia ni msimamizi wa mchezo huo Bw.Salum Mvuta

Filed under: Uncategorized | No Comments

KAMA NIKIDONDOSHA BADO NAWEZA KUILA…??

Watu wengi tumezowea ya kuwa chochote unachokula kiki dondoka basi hakifai kuliwa tena.Ambapo hapo awali watafiti walisema kama utaweza kuokota ulichokidondosha ndani ya sekunde tano basi hakifaa kulika.

Sasa baada ya  tafiti mbalimbali kufanyika kwa upana zaidi imegundulika si kweli, bali itategemeana na mazingira yaliyopo. Inasemekana vijdudu viauwezo wa kuhamia katika chakula  kilicho dondoka  ndani ya sekunde 3 sana sana kama chakula hicho kina hali ya majimaji na hali halisi ya uchafu ya sehemu kilipo dondokea. Mpaka sasa wanasayansi wanabishana kuhusiana na hali hiyo.

Mwisho wa siku uwamuzi wa kula unabakia kwako wewe mlaji, je unamoyo gani wa kuokota msosi ulio dondoka na kuula ukizingatia njaa uliyokuwa nayo na kiasi cha fedha ulichotumia kununulia.?

Filed under: Uncategorized | No Comments

IMAGE OF THE DAY….!!!

Mheshimiwa,mfanyabishara maarufu na mwanaspoti kijana Mohammed Dewji.

“Ni muhimu katika maendeleo ya biashara yako ukajitahidi kwa kadri ya uwezo wako kuwafahamu wateja wako vizuri.


Kama hautaweza kuwajua wateja unaho wahudumia je utaweza fahamua vipi kama unawaridhisha katika mpango mzima wa kuwahudumia?.


Kwa sababu maendeleo biashara yako yanategemeana na wewe  kufanikiwa kuwaridhisha wale unaowapa huduma.


Kwa hiyo unatakiwa kuwatambua wateja wako ni wapi na wanatabia gani na nikipi wanauwezo wa kununua. Mimi nalitambua hilo ndio maana mpaka leo naweza kuwa hudumia wateja wangu si tu kwa ubora wa juu bidhaa bali pia kwa usalama mkubwa”.- Mohammed Dewji.

Filed under: Uncategorized | No Comments